Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

VIDEO: Goli mbili za Sanchez zilivyomnyamazisha Suarez (Chile vs Uruguay)

$
0
0

alexis

Star wa Chile Alexis Sanchez hakuwepo kwenye kikosi kilichotoka suluhu na Colombia Alhamisi iliyopita lakini usiku wa jana alikuwa fiti kwenye mechi muhimu dhidi ya Uruguay ya kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia.

Uruguay walianza kupata bao la kuongoza likifungwa na Edinson Cavani lakini nyota wa Arsenal alimaliza kipindi cha pili akiwa ameshaweka kambani bao mbili safi baada ya Edu Vargas kusawazisha.

Chile wapo kwenye hatari ya kukosa michuano ya Kombe la Dunia 2018 (wapo nafasi ya nne a pointi 20 baada ya mechi 12) lakini mpambanaji Alexis Sanchez hakukubali kutoka nje ya uwanja bila kupasia nyavu.

Alexis Sanchez alipokea mpira wa kurushwa kisha akawahadaa mabeki na kuachia kiki kali kufunga bao lake la kwanza likiwa ni bao la pili kwa Chile kwenye mchezo huo.

Star huyo mwenye miaka 27, alipenya mbele ya mabeki wawili kisha kupachika bao lake la pili.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>