Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Uamuzi wa Zaha ili kucheza timu ya taifa ya Ivory Coast

$
0
0

wilfriedz-zaha

Winga wa Crystal Palace Wilfred Zaha amerejesha maombi FIFA ya kubadili utaifa wake kutoka England kwenda Ivory Coast.

Zaha ambaye alizaliwa Abidjan lakini akakulia England, ameshaitumikia England kwenye michezo miwili ambayo yote ilikuwa ni ya kirafiki anaruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za FIFA.

Zaha, 24, atakuwa na zifa za kuitumikia Ivory Coast kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika.

Michuano hiyo ambayo itafanyika Gabon kuanzia Januari 14 mwaka ujao tunaweza kumshuhudia Zaha na kukosekana kwenye kikosi cha Palace kwa zaidi ya wiki sita ndani ya msimu huu.

wilfried-zaha-1

Taarifa kutoka Shirikisho la soka la Ivory Coast inasema Zaha ametuma barua FIFA siku ya Jumapili kuomba kubadili uraia.

Kocha wa Palace Alan Pardew amesema Zaha ameshawishiwa na watu wanaomzunguka ili abadili utaifa au kutokana na kutoitwa kwenye kikosi cha England.

Alitokea benchi na kucheza dakika 15 za mwisho wakati England ikipata ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Scotland kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Wembley August 2013.

Zaha alijiunga na Palace kwa mkataba wa kudumu akitokea Manchester United February 2015 alikitumikia kikosi cha England cha U-21  katika michezo 13.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>