Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Shabiki wa Chelsea anusurika kifo nje ya Stanford Bridge.

$
0
0

screen-shot-2016-11-28-at-6-17-05-pmMechi ya Chesea Vs Spurs haikuisha kwa furaha kwa mashabiki wote wa Chelsea. Wengine walipata matokeo ya mechi wakiwa hospital kuokoa maisha yao.

Shabiki mmoja wa Chelsea ambae alikua na wakina dada wawili wakielekea kwenye mechi dhidi ya Spurs alipigwa na kitu cha chuma kichwa na kudondoka hapo hapo.

Bahati nzuri wakina dada wawili aliokua nao walipiga kelele nyingi huku jamaa huyo akitoka damu kichwani. Shabiki huyo maarufu anayemiliki ticket ya msimu mzima alikimbizwa kwenye hospital ya Westminster.

Club ya Chelsea imethibisha tukio hilo baada ya kupata taarifa polisi na wao binafsi wamefanya ufatiliaji kwa shabiki wao huyo ambaye amenunua ticket za msimu mzima. Msemaji wa Chelsea alisema,“Tumepokea taarifa hizi na tumeambiwa kwamba alilengwa na mtu ambaye bado hajajulikana”.

Ni kawaida sana kutokea fujo za hapa na pale ikitokea mechi ya Spurs na Chelsea. Kwenye mechi hiyo imeendelea kuiweka pazuri Chelsea baada ya kushinda 2-1.

screen-shot-2016-11-28-at-6-16-59-pm


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>