Kocha wa sasa wa Manchester City alishinda kila taji akiwa na Barcelona kabla hajaenda Bayern Munich. Mwaka huu Barcelona wamesajili Samuel Umtiti ambaye alikua anaifatilia Barcelona tangu ikiwa chini ya Frank Rijkaard.
Mchezaji huyo mwenye miaka 23 amesema kwamba alikua anapenda style ya soka ya Barcelona wakati ipo chini ya Frank Rijkaard kwa muda wote wa 2003 hadi 2008. “Frank Rijkaard alikua kocha ambae nilimpenda na niliipenda Barcelona kwa style ile ya uchezaji. Jinsi wachezaji walivyokua wanakaa na mpira na kwenda na mpira, hakuna timu nyingine ambayo ilifanya vile”, Umtiti aliliambia gazeti la France Football.
Aliendelea kusifia kipindi cha Rijkaard na kuponda kipindi cha Pep,“Kulikua na utamaduni mzuri wa kushinda kipindi kile, wachezaji hawakuonyesha kama wametosheka na mafanikio na sikukosa karibia kila mechi yao. Sasa baada ya hapo kikaja kipindi ambacho hakikunivutia kabisa. Niliwaaambia marafiki zangu kwamba hii sio style ya Barcelona ninayoikubali. Ilikua haivutii kuangalia kabisa lakini angalau Barcelona imebadirika sasa hivi”.
Maoni yako ni yapi kati yaBarcelona ya Rijkaard na Barcelona ya Pep. Ipi ilikua inavutia kuangalia?. Nipe maoni yako kwenye comment.