Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Kaburu kasema hajamuona ‘mkata umeme,’ amemuona ‘kishoka’

$
0
0

img_0189

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba SC  Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema hajamuona kiungo wa Yanga Justine Zulu ambaye kwa sasa ni maarufu kwa jina la ‘mkata umeme’.

Badala yake Kaburu amesema aliyemuona ni ‘kishoka’ (mafundi umeme wababaishaji) au wakuungaunga.

“Nienda uwanja wa Uhuru kumuangalia mtani wangu yupoje, lakini sijamuona huyo mkata umeme nimuona ‘kishoka’ tu,” amesikika Kaburu kupitia kipindi cha Sports Extra kilichokuwa kinaruka moja kwa moja kutoka G-Five, Kigamboni.

Justine Zulu amecheza kipindi cha pili kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya JKU, alisajiliwa kutoka klabu ya Zesco United ya Zambia na kuungana na kocha wake wa zamani George Lwandamina waliokuwa pamoja toka Zambia.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>