Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba, ameonekana tena kwenye mchezo wa kirafiki wa Yanga wakati wanaikabili JKU kutoka visiwani Zanzibar.
Mh. Nchemba ameonekana kwenye mechi nyingi za Yanga lakini inawezekana watu wengi walidhani labda asingetokea kwenye mchezo wa kirafiki lakini mpenzi huyo wa mabingwa watetezi wa VPL akatokea uwanjani dakika chache baada ya mechi kuanza.
Kama unakumbuka vizuri, Mh. Nchemba alipamaba kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Pluijm anabadili uamuzi wake wa kujiuzulu kuifundisha Yanga baada ya tetesi kumfikia kuwa, Yanga imeingia mkataba na kocha mwingine bila yeye kujua.