China Super League au unaweza kuiita kama ligi ya pesa nyingi inafanya maajabu mengine kwa kumnunua mchezaji wa Chelsea Oscar kwa kiasi cha £52million.
Midfielder huyu kutoka Brazil hajaanza kwenye Premier League tangu kati ya mwezi wa tisa. Sasa hivi amepewa nafasi ya kwenda kucheza pamoja na striker Hulk kwenye club ya Shanghai SIPG inayonolewa na Andre Villas Boas.
Hulk ambae anashikilia rekodi ya gharama kubwa ya usajili kwenye ligi hiyo ya China inasemekena analipwa kiasi cha pound 320,000 kwa wiki. Oscar atakua star wa tatu kujiunga na ligi ya China kutoka Chelsea baada ya kuanza Demba Ba na Ramires. Akiwa ndani ya Chelsea amefanikiwa kucheza michezo 203 na kufunga magoli 38.
Wachezaji wengine maarufu waliopo kwenye ligi ya China ni Gervinho, Stephane M’bia,Obafemi Martins, Demba Ba, Gael Kakuta,Hulk, Ramires na wengineo.