Kupitia ukurasa wa Instagram ya afisa habari wa Simba Haji Manara, kuna picha ambayo inasambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha rais wa klabu hiyo akikabidhi mkataba wa usajili kwa mshambuliaji wa Stand United Pastory Athanas.
Bado haijafahamika striker huyo amesajiliwa kwa kiasi gani na amepewa mkataba wa muda gani kuitumikia Simba SC.