Ikiwa dirisha dogo linafungwa usiku wa December 15, klabu ya Yanga imeweka wazi wachezaji iliowasajili kuingia katika klabu hiyo pamoja na waliotoka ndani ya klabu hiyo inayopambana kutetea mataji yake ya VPL na FA.
Walioingia
Yanga imetumia dirisha dogo kuwasajiliwa wachezaji wawili, waliosajiliwa ni Justine Zulu kutoka Zambia na Emanuel Martin kutoka JKU ya Zanzibar.
Waliotoka
Mbuyu Twite ni mchezaji pekee aliyeondoka Yanga katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili. Kwa mujibu wa Makamu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedith, Twite alimaliza mkataba wake na klabu ikaamua kumwacha aondoke kama mchezaji huru.
Hakuna mchezaji yeyote aliyetolewa kwa mkopo na klabu ya Yanga na klabu hiyo imeshafunga usajili wake wa dirisha dogo.