Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

OFFICIAL: Ngasa amerejea VPL

$
0
0

ngasa-3

Mrisho Ngasa amefanya mazoezi kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Mbeya City chini ya kocha mkuu Kinnah Phiri katika harakati za kujiandaa na mechi yao ya kwanza ya mzunguko wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

ngasa-2

Ngasa ambaye hivi karibuni alivunja mkataba na klabu ya Free State Stars ya South Africa, aliibukia uarabuni ambako nako hakudumu na hatimaye kurejea Bongo amesaini mkataba wa mwaka mmoja utakaomfanya avae jezi za timu hiyo ya Halmashauri ya jiji la Mbeya.

ngasa-1

Ngasa ambaye atakuwa akivaa jezi namba 35 akiwa kwenye kikosi cha Mbeya City huenda akacheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Mbeya City wakati kitakapo ialika Kagera Sugar FC ya Bukoba, Kagera.

ngasa

Picha kwa hisani ya Fahari News na Mbeya City FC


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>