Star wa Real Madrid na mshindi wa Ballon d’Or 2016 Cristiano Ronaldo amefunga goli la 500 wakati Real Madrid ikipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Club America katika mchezo wake wa nusu fainali ya kombe la vila bingwa vya dunia huko nchini Japan.
Magoli 500 aliyofunga Ronaldo ni mjumuisho wa magoli yote aliyowahi kufunga katika vila vitatu ambavyo amewahi kuvitumikia kwa nyakati tofauti.
Ameshafunga magoli 377 akiwa amevalia uzi wa Real Madrid, alifunga magoli 118 wakati anacheza Manchester United huku akiwa amefunga magoli matano wakati akiwa mchezaji wa Sporting Lisbon.
Madrid itacheza mchezo wa fainali ya Club World Cup siku ya jumapili dhidi ya Kashima Antlers.
Vilabu vitano ambavo Ronaldo amevifunga magoli mengi ni pamoja na;
- Sevilla – 22 goals
- Getafe – 20
- Atletico Madrid – 18
- Celta Vigo – 17
- Barcelona – 16