Barcelona wamefanikiwa kupata saini muhimu ya mchezaji wao Luis Suarez na kujihakikishia kwamba atakuwepo na club hiyo hadi mwaka 2021. Suarez alikua ni mmoja ya wachezaji ambao wanatakiwa sana kuongeza mkataba wake kutokana na mchango mkubwa ambao anao kwenye club hiyo.
Inasemekana kwenye mkataba huu mpya buy-out clause yake ni kiasi cha pound 167 milioni. Hasi sasa mchezaji huyu wa kimataifa wa Uruguay ameshafunga mata 97 na kutoka asisst 48 tangu ajiunge na Barcelona mwaka 2014.
Suarez baada ya kutangazwa kwamba atacheza kwa miaka mitano zaidi ndani ya Barcelona alisema,“Najiskia vizuri sana kuhusu mimi kuwa sehemu ambayo nahitaji kuwepo. Uhusuiano wangu na club ni mzuri sana. Ni maamuzi ambayo wote tulitaka kufikia. Mchezaji yoyote angependa kumaliza maisha yake ya soka kwenye club anayoipenda”