Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

HABARI MPYA KUHUSU HALI YA HAMISI KIIZA, JE ATACHEZA AU HATOCHEZA DHIDI YA COASTAL UNION?

$
0
0
Hamisi Kiiza, mshambuliaji wa klabu ya Simba
Hamisi Kiiza, mshambuliaji wa klabu ya Simba

Kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’ Simba kikiwa katika maandalizi ya kuwavaa ‘wagosi wa kaya’ Coastal Union siku ya Jumatano, hali ya majeruhi Hamisi Kiiza imezidi kuimarika na yupo tayari kuongoza mashambulizi ya kikosi cha Dylan Kerr.

Mtandao huu umemtafuta daktari wa Simba SC Yasin Gembe ambaye amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kusema baada ya kupata matibabu, raia huyo wa Uganda yuko tayari kucheza mchezo dhidi ya Coastal Union.

“Kiiza sasa hivi yuko sawa, tangu alipopata ‘injury’ alikuwa anahitaji wiki tatu au zaidi lakini ndani ya wiki tatu ameonesha ‘recovery’ ya kutosha, ameshaanza mazoezi tangu wiki iliyopita kwahiyo mwalimu kama atamuhitaji anaweza kumtumia kwenye mechi ijayo”, amesema Gembe.

“Mbali na Kiiza wachezaji wengine wako vizuri isipokuwa kwa Faki ambaye alikuwa na maumivu ya goti kwa muda mrefu na ni mchezaji pekee ambaye hayupo kwenye kambi lakini wengine wote wapo kambini”.

Urejeo wa Hamisi Kiiza kwenye kikosi cha Simba ni habari njema kwa mashabiki wa Simba ambao walimkosa kwenye michezo mitatu iliyopita.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>