Hakuna timu inayopenda kupoteza mchezo hasa mechi ya fainali huku kombe likiwa limewekwa tayari kwa ajili ya bingwa.
Hiki ndicho kimewatokea Simba usiku wa Ijumaa January 13 kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Wakiwa wanajua kabisa wakishinda mechi watakuwa mabingwa wapya na kukabidhiwa kombe la Mapinduzi 2017, Simba walijikuta wakiishia kuhuzunika kutokana na kupoteza mchezo wao wa fainali mbele ya Azam.