Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Costa hayupo kwenye mechi dhidi ya Leicester…ni upenyo au?

$
0
0

Screen Shot 2017-01-14 at 3.30.49 PM

Diego Costa ni kati ya wachezaji waliokuwa wakorofi sana.Msimu huu baada ya kuja kwa kocha Antonio Conte alionekana kutulia,Costa inasemekana alikuwa kati ya wachezaji waliokuwa kwenye mgomo uliosababisha Josee Mourinho kutimuliwa.Wakati wa dirisha lililopita la usajili Costa inasemekana alikuwa karibu kurudi katika timu yake ya zamani ya Athletico Madrid.

Toka kuwasili kwa kocha Antonio Conte alifanikiwa kuleta muungano katika timu.Wachezaji walionekana kujituma na kuwa kitu kimoja.Chelsea wanaoonekana kama timu bora kwa sasa Uingere,na mmoja kati ya wachezaji walioifanya Chelsea kuongoza ligi ni mshambuliaji wao huyu Diego Costa.Costa akiwa ameweka kimiani magoli 14 na amewawezesha kuongoza msimamo wa ligi.

 

Lakini sasa uhusiano na umoja uliokuwapo kati ya Chelsea na Costa umeingia mashakani.Hii inakuja  baada ya kocha Antonio Conte kumuacha Costa katika kikosi kinachoenda kucheza na Leicester City.Costa inasemekana hajafanya mazoezi na timu hiyo kwa siku tatu zilizopita kutokana na majeruhi.Kitendo cha Costa kutemwa kinaleta hali ya sintofahamu kuhusu future yake Stamford Bridge.

 

Lakini vyombo bingi vya habari vinasema Conte amemuacha Costa kwa kuwa hayuko fiti kisaikolojia.Hii inatokana na ofa ambayo Costa amepewa toka timu ya Tianjin Quanjian na Shanghai SIPG ya China.Dili kati ya Costa na Wachina hao inasemekana limekwenda mbali kwani wawakilishi wa Costa wako nchini China kusikiliza ofa za timu hizo.

 

Chelsea wanasemekana wanataka kumuongezea mkataba msanii huyo.Kocha wa timu hiyo Antonio Conte hawezi kuwa na furaha kumkosa Costa,kwani Costa ni mchezaji mubimu sana katika kikosi chake haswa wakati huu ligi ikiwa katika raundi ya pili.Timu za China msimu huu zinaonekana kupiga hodi Epl haswa Chelsea.Hadi sasa Oscar ameshaenda Shanghai SIPG,John Obi Mikel akienda Tianjin Teda huku pia wakiwa wamemuuza Ramires aliyeenda Jiangsu Sunning,sasa wamepiga hodi tena kwa Costa.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>