Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema huwa hakai na kufikiria kuhusu kibarua chake Stamford Bridge huku akiviambia vyombo vya habari kwamba vinajaribu kuweka presha kwake lakini havitaweza.
Chelsea iko katika kipindi kigumu tangu kuanza kwa msimu huu, na mpaka sasa wanashikilia nafasi ya 15 huku wakimenyana na Liverpool mchana wa leo Stamford Bridge.
Akiulizwa kuhusu kama kapewa guarantee na mabosi wake Jose amesema hawezi kusema kuhusu hilo kwani yeye sio mtu wa dunia ya leo na kwamba anaishi kwenye ulimwengu asiostahili kuwepo.
Kuhusu kutoa ahadi kama ana uhakika wa Chelsea kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao, Mourinho pia amegoma kuahidi chochote huku akisema, Liverpool ni timu kubwa lakini Manchester United ni kubwa zaidi… Lakini zote zilimaliza msimu wa mwaka jana bila kombe hata moja.
Mourinho haoni tatizo wala ajabu kwa timu yake kumaliza msimu bila kombe akifananisha na jinsi ilivyovitokea vilabu vingine vikubwa duniani.