
Amir Maftah ni jina kubwa kwenye tasnia ya soka la Tanzania, ni mchezaji aliyewahi kucheza kwenye vilabu tofauti vinavyoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa mafanikio makubwa kwenye miaka ya nyuma kidogo.
Jina la Maftah kwasasa linafifia kwenye soka la Tanzania na ndio kitu haswaa kilichoifanya timu ya Dauda tv kumtafuta Amir Maftah na kufanya nae mazungumzo kujua nini kimemsibu.
Maftah kwa sasa anacheza kwenye timu ya Friends Rangers ya Magomeni inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara (FDL) lakini anasema muda mwingi ameuwekeza kwenye masomo akiwa anasoma kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (University Computing Centre-UCC) tawi la Mbezi Beach.
Maftah amesema maisha yamebadilika na hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya aingie darasani kupiga kitabu kidogo ili hata kama akiachana kabisa na soka basi ajishughulishe na mambo menine nje ya mchezo huo ili aweze kujipatia kipato na kuendesha maisha yake na familia.
Lkini akasisitiza kuwa, baada ya kumaliza masomo yake anataka kucheza kwa msimu mmoja kwenye klabu ya ligi kuu Tanzania bara na kama ikishindikana basi atakwenda kucheza soka lake Dubai ambako alishawahi kucheza miaka ya nyuma kabla ya kuamua kutundika rasmi daruga na kuachana na soka kabisa.
Kwasasa anaishi Magomeni-Mapipa jijini Dar es Salaam pamoja na familia yake ambapo ana mke na watoto watatu.
Mtoto wa kwanza wa Maftah anaitwa Neymar jina la Star wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil. Maftah amesema aliamua kumpa mwanae jina hilo kwasabu wakati mtoto huyo anazaliwa, ndio kipindi ambacho Neymar Jr alianza kuwa juu kwenye mchezo wa soka.
“Nilimwita Neymar kwasababu kipindi ambacho anazaliwa ndio Neymar alianza kuwa juu, mama yake alikuwa hamjui Neymar lakini alipokua akiangalia TV akimuona anauliza huyu nani, namwambia anaitwa Neymar, basi tulivyopata mtoto akasema mwangu nataka aitwe Neymar basi ikawa hivyo”, amesema Maftah.
Mto wa pili wa Maftah anaitwa Nizar jana jingine la star wa soka wa Tanzania ambaye amewahi kucheza soka kwenye ligi ya Marekani lakini pia timu ya taifa ya Tanzania na vilabu vya kadhaa vya ligi kuu ya Vodacom lakini kwasasa yupo Mwadui FC ya Shinyanga.
Maftah mesema aliamua kumpa mwanae huyo jina la Nizar kwasababu Nizar Khalfani ni rafikiake wa karibu kwahiyo aliambua kufanya hivyo kwa ajili ya kufariji rafikiyake.
“Nizar ni rafikiyangu na mtu wa karibu sana kwangu, ni ngugu yangu kwahiyo nilimpa jina hilo kwa ajili ya kumfariji rafikiyangu”.
Angalia video hapa chini ambapo Maftah ameeleza mambo mengi kuhusu maisha yake ya soka.