Golden State warriors wameendelea kuthibitisha kuwa wao ni bora baada ya kuifunga New Orleans Pelicans mara mbili ndani ya michezo yao mitatu ya ufunguzi msimu huu. Wakitoka kuipiga Houston Rockets, alfajiri ya leo wameinyanyasha Pelicans huku Curry akiwa hashikiki. Wameshinda 134-120
“Imefika mahali ambapo sasa inabidi niwafanye vijana wangu waweze kucheza kwa kuzungusha mpira zaidi. Leo hatukuwa vizuri kiushambulizi na tulikwama mara kwa mara ,” kocha wa Pelicans Gentry alisema. “Nadhani tulicheza kwa ubinafsi kidogo katika ushambuliaji, kuwaambia ukweli . ”
Curry alifunga pointi 53 , na kuufanya mchezo uliokuwa unaonekana mgumu kuwa rahisi, huku akifunga point katika robo ya tatu.Golden State Warriors imeendeleza rekodi ya kutofungwa kwa kuitandika Pelicans 134-120 nyumbani kwao. Pelicans hawajashinda mchezo wowote mpaka sasa.
“Mara zote nimekuwa na ujasiri ,” alisema Curry , mshindi wa tuzo ya NBA MVP . “Kikubwa tu ni kupata ubora kama mchezaji na kujaribu kukipeleka katika ngazi nyingine. Hicho ndicho ninachojaribu kufanya mwaka huu, nina heri kuwa na afya.
Draymond Green alifunga pointi 21, na Klay Thompson aliongeza 19 kwa mabingwa watetezi Golden State, ambayo imeshinda michezo yake ya kwanza mitatu msimu huu.
Anthony Davis alikuwa na pointi 26, 15 rebounds na block mbili Pelicans ambayo inaandamwa na majeruhi lukuki. Imepoteza mechi zao tatu za mwanzo chini ya kocha mpya Alvin Gentry . Miwili ikiwa dhidi ya Golden State Warriors, ambapo Gentry alikuwa kocha msaidizi msimu uliopita.
HIGHLIGHTS