Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MOISE KATUMBI: WACHEZAJI WOTE WANGEKUWA NA NIDHAMU KAMA SAMATTA NA ULIMWENGU, SOKA LA AFRIKA LINGEFIKA MBALI

$
0
0
Shaffih Dauda (kushoto) akifanya mahojiano maalumu na rais wa TP Mazembe Moise Katumbi (kulia)
Shaffih Dauda (kushoto) akifanya mahojiano maalumu na rais wa TP Mazembe Moise Katumbi (kulia)

Wakati viongozi wa mpira Tanzania wakipiga kelele kuhusu wachezaji kuwa na nidhamu, rais wa TP Mazembe Moise Katumbi amesema, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ni wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu na hiyo inafanya yeye kuwatazama kawa watoto wake na kuongeza kuwa, kama wachezaji wengine wa Afrika wangekuwa na nidhamu kama ya vijana hao basi Afrika ingefika mbali kisoka.

Klabu ya TP Mazembe inawachezaji wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Zambia, Ghana, Malawi, Mali, Tanzania pamoja na wenyewe Congo DR lakini sifa hizo zimekwenda kwa vijana wawili kutoka Tanzania.

Katumbi pia amezungumzia kuhusu mpango mzima wa Samatta kutimkia kucheza soka Ulaya na tayari kunatimu nyingi zimeshaonesha nia ya kutaka kumnasa huku akisisitiza kuwa, atahakikisha Samatta anapata timu nzuri ili akaitangaze vyema TP Mazembe na nchi yake Tanzania.

Shaffihdauda.co.tz: Unawazungumziaje Mbwana Samatta pamoja na Thomas Ulimwengu?

Katumbi: Kabla ya kuzungumzia kiwango cha Samata na Ulimwengu jambo la kwanza ni nidhamu, hawa ni wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu kwenye timu yetu. Sijawahi kusikia tatizo lolote, kwanza hawa ni kama watoto wangu. Wanaelimu nzuri sana ya nidhamu kama wachezaji wote wa Afrika watakuwa na nidhamu kama hawa vijana, basi soka la Afrika litafika mbali sana.

Lakini nadhani muda mfupi ujao Samatta ataelekea Ulaya tayari kuna timu nyingi ambazo zinamuhitaji lakini ameshafanya kazi kubwa hapa TP Mazembe sasa muda huu ni wake kwenda Ulaya kufurahia maisha yake ya soka.

Shaffihdauda.co.tz: Hiyo inamaasha sasa uko tayari kumwachia Samatta aondoke kama kuna klabu yoyote kutoka Ulaya itakuwa inamuhitaji?

Katumbi: Tayari kuna timu nyingi ambazo zinamtaka Samatta na mimi kama mzazi nataka aende kwenye timu ambayo atapata mafanikio sio kumwacha aende kwenye timu ilimradi tu ipo Ulaya. Nataka akalitangaze vizuri jina la TP Mazembe na Tanzania na watanzania wajivunie kijana wao kucheza Ulaya.

Shaffihdauda.co.tz: Unaweza ukazitaja baadhi ya timu za Ulaya zinazo muwania Samatta?

Katumbi: Siweze kuzitaja kwa sasa, kwasababu bado ni siri.

Shaffihdauda.co.tz: Huko mtaani watu wamekuwa wakikuzungumzia sana wakidai unafaa kuwa rais ajae wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, uko tayari kuwatumikia watu wa Congo DR?

Katumbi: Kwasasa, tuongelee kwanza TP Mazembe, tutaongea wakati mwingine tutaongea kuhusu siasa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles