Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Je Messi anaweza kutamba Britannia kwa Stoke? Barca ingeweza kutwaa EPL? Majibu ameyatoa Pique hapa

$
0
0

“Yeah, but can he do it on a cold rainy night in Stoke. (Ndio, lakini anaweza kufanya anayofanya kwenye usiku wa baridi na mvua pale Stoke?”

Huu ni msemo maarufu kwenye soka unaotumika kwa mastaa wa nje ya England ambao bado hawajacheZa katika EPL.  

  Kwenye mahojiano na gazeti la Telegraph , mlinizi wa Barcelona  Gerard Pique amekaririwa akisema kwamba hata mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kutokea Leo Messi angepata taabu sana kucheza kwenye dimba la Britanna, huku pia akisema kwamba hata mabingwa wa ulaya wasingekuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa wa Premier League. 

Rekodi ya mabingwa wa Ulaya na Spain mbele ya timu za England ni nzuri sana lakini Pique anaamini kungekuwa na nafasi finyu sana  kwa Barcelona kuwa mabingwa wa EPL kama ingetokea wangekuwa wanashiriki ligi ya England, labda ingewezekana baada ya msimu kadhaa baadae. 

“Nadhani kama Barcelona au Real Madrid wakienda kwenye  Premier League basi mwaka wa kwanza wa kucheza kule, hawatokuwa na nafasi ya kushinda ubingwa,” Pique ameiambia Telegraph. 

  Kweli? Akauliza mwandishi wa gazeti hilo. 

“Yes, nadhani hivyo, kwa sababu kwenda kucheza ugenini na timu aina ya Stoke au timu nyingine – ni ngumu sana kupata matokeo. Huu ni mjadala ambao tunaweza kukesha tukijadili. Hata Man United au Chelsea wakienda Spain kesi itakuwa ile ile. Nafasi ya kutwaa ubingwa ni finyu.” 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>