Miami Heat Ilitangaza Jumanne kwamba imefanya biashara ya mkongwe point guard wao Mario Chalmers kwa kumpeleka kunako klabu ya Memphis Grizzlies . Katika hiyo wachezaji wanne wamehusika katika mabadilishano au biashara hiyo.
Miami Heat imemtoa Chalmers pamoja na fowadi wao James Ennis kwa Grizzlies na kuwapata guard Beno Udrih na fowadi Jarnell Stokes .
Vyanzo vya Ligi vinadai kuwa Miami Heat iliiomba Grizzlies muda zaidi, baada ya pande zote kukubaliana katika kanuni na mfumo wao wa biashara ya Jumanne utakavyokuwa. Hii ilikuwa ni kujaribu kupata timu ya tatu ili kujaribu kunyonya makali ya mkataba.
Mpango ulikuwa ni timu ya tatu kumchukua ama Udrih au Stokes . Kisha timu hzi ziliamua kuendelea na biashara yao Jumanne usiku, baada ya kukosekana timu ya tatu ambayo ingekubali kujiunga katika dili hilo, na kuleta kilele cha biashara hiyo ambayo mazungumzo yake yamekuwa yakiendelea kwa siku kadhaa.
“Hii ni siku ngumu kwangu mwenyewe na Miami Heat kwa ujumla katika biashara hii ya Mario Chalmers na James Ennis, ” rais wa Heat Pat Riley alisema katika taarifa ya timu. ” Mario alikuwa ni sehemu ya kikosi kilichoshinda ubingwa mara mbili na sisi, na Ennis ni mchezaji kijana na imara sana.
Lakini ni sehemu ya biashara , na ilikuwa hoja muhimu kufanya kwa sababu ya nafasi za nyuma kujaa wachezaji. Tunahisi kwamba ni kwa maslahi bora ya Mario , na tunataka apate kuwa na mafanikio na kuwa sehemu ya timu nzurihuko aendako.
Hatuna la zaidi isipokuwa kumtakia kila lililo jema na la kheri ” Kwa Chalmers kuondoka na kuelekea Grizzlies, Dwyane Wade , Chris Bosh , Udonis Haslem na Andersen ni wachezaji pekee waliobaki ambao walikuwepo wakati Miami inashinda ubingwa wake wa mwisho wa mwaka 2013. .
“Siku kama hii si ya furaha kabisa, ” Wade alisema. ” Rio (Mario Chalmers) ni zaidi ya ndugu kwetu na ni kaka yetu pia. “