Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

AIRTEL YATWAA VIKOMBE VINNE AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa (kushoto) akimkabithi kikombe Afisa masoko na biashara wa Airtel, Emmanuel Raphael mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka mshindi wa pili  katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ya mwaka huu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepokea vikombe vinne katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kufatia ubora wake katika kutoa huduma na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake.

Maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mashariki ni maarufu kwa kuonyesha aina mbalimbali za bidhaa ikiwemo bidhaa za matumizi ya kawaida na ya viwanda, huduma, mashine na teknologia.

Na maonesho haya yametoa fursa ya kukutanisha wadau pamoja na kubadilishana uzoefu wa kibiashara katika nchini za ukanda wa mashariki.

Akiongea wakati wa halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Abbas Musa alisema;”Maonyesho haya yana lengo la kuwapatia makampuni yaliyoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki fursa ya kujitangaza na kukuza biashara zao lakini pia kuwapatia nafasi ya kuboresha mahusiano ya kudumu na wateja wao. Leo najisikia furaha kuwazawadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuonesha ubora wake katika huduma, bidhaa, tecknologia za kibunifu na kwa kuwa washindi wapili katika maonyesho  ya mwaka huu”.

Aliongeza kwa kusema; ”Airtel imedhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma za kibunifu na za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na kutokana na hilo tumeona ni muhimu kuwapongeza na kuwazawadia kwa jitihada zao”.

Kwa upande wake Afisa Masoko na bidhaa wa Airtel, Bwana Emmanuel Raphael alisema; “huu ni mwaka wa tano mfululizo sasa kwa Airtel kushiriki katika maonesho haya tukiwa na lengo la kufikia wateja wetu, kutoa elimu ya huduma na bidhaa tunazotoa pamoja na kuboresha mahusiano nao.

Wafanyakazi wa Airtel kwa pamoja wakiwa na makombe yao mara baada ya kukabithiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara Uledi Abbas Musa mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuibuka washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya Afrika Mashariki ya mwaka huu

Maonyesho haya pia yamekuwa ni fursa muhimu kwetu kuonyesha bidhaa na huduma zetu za kibunifu na za kisasa na pia ni nafasi pekee ya kushirikiana na makampuni mengine yanayoshiriki kila mwaka”.

“Napenda kuwashukuru waandaaji wa maonyesho haya kwa kutambua na kuona mchango wetu na tunahaidi kuendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu.”

Katika halfa hiyo, Airtel ilipokea makombe manne ya ubora katika vipengele vya  namba moja kwenye kutoa huduma, namba moja katika sekta ya mawasiliano, namba moja katika teknologia ya mawasiliano ya habari na namba mbili katika maonesho ya mwaka huu. Nchi zilizo shiriki katika maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda and Burundi.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>