Manchester City leo wamejipoza kwa ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Southampton mchezo ulipigwa kwenye dimba la Etihad, kabla ya mchezo huo Man City ilikuwa na kumbukumbu ya vipigo kutoka kwa Liverpool kwenye mchezo wa ligi ya England kabla ya kuchapwa na Juventus kwenye michuano ya Ulaya.
Kelvin de Bruyne alianza kuifungia City bao la kwanza dakika ya tisa huku Fabian Delph akipachika bao la pili dakika ya 21 kipindi wakati Kolarov akipachika bao la tatu dakika ya 70 na kuihakikishia ushindi timu yake.
Bao pekee la kufutia machozi la Southampton limefungwa na Shane Long 50 na kufanya dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa City kutwaa pointi zote tatu na kufikisha jumla ya pointi 29 baada ya kucheza mechi 13 na kupata nafasi ya kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa na Leicester City wenye pointi 29 pia wakiwa nafasi ya pili baada ya sare ya kufungana goli 1-1 na Manchester United .