Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Manchester United ‘Inayoboa’ Itaweza Kutwaa Ubingwa wa EPL? – Majibu yangu Haya Hapa

$
0
0

Manchester United waliikosa nafasi ya kupanda juu ya kilele cha Premier League baada ya mechi nyingine ya sare waliyocheza katika kiwango cha chini vs Leceister City jumamosi iliyopita.

United wamebakia kuwa katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City na Leicester – lakini wanausaliti utamaduni wao wa hivi karibuni kwa aina ya mchezo wanaouonyesha, lakini Je wanaweza kushinda ubingwa kwa mchezo wanaocheza hivi sasa?

  Ni sahihi kuiita Man United ‘boring’?

Ni swali ambalo lisingeweza hata kufikiriwa katika siku za ushindi za uongozi wa Sir Alex Ferguson wakati kila mechi ya United – ilikuwa inahusisha mashambulizi ya hatari na muda wote timu ilionekana kuusaka mafanikio kwa kushinda mechi.

Kocha wa zamani wa Manchester United Rene Meulensteen hivi karibuni alielezea namna Ferguson alivyokuwa analichukuliw suala
la kushambulia.

“Sir Alex alikuwa wazi kabisa kuhusu suala
hili. ‘Tunataka kuwa na mafanikio, tunataka kushinda mechi na makombe lakini tuna jukumu la kuwaburudisha mashabiki wetu.”

United ya miaka kadhaa iliyopita ilikuwa na utamadunia wa kucheza soka la kusisimua – lakini kumekuwepo na na kutoridhishwa kwa aina ya mchezo ambao unaonyeshwa na vijana wa Louis Van Gaal, ambaye uteuzi wake ulikuja baada ya msimu wa ovyo chini ya utawala wa David Moyes.

Takwimu zinatetea kutoridhishwa kwao na malalamiko yao dhidi ya timu yao inavyocheza kinyume na utamaduni.  

TAKWIMU ZA USHAMBULIAJI ZA UTD KUTOKA 2010-16


Katika mechi 14 za Premier League  msimu huu, wamefunga magoli 20 kutoka katika mashuti 146 na 53 tu ndio yaliyolenga magoli. Hata kwenye msimu wa balaa wa Moyes mwaka 2013-14, walifunga mara 22 baada ya kucheza idadi sawa ya michezo (14). 

Katika msimu wa mwisho wa Ferguson ambao walishinda taji 2012-13, mpaka kufikia hatua hii kwenye msimu walikuwa tayari wamefunga magoli 33 kutoka kwenye mipira 229 iliyopigwa langoni huku 84 ikilenga goli. 

 
Wakati kinda Anthony Martial aliposajiliwa kwa  £36m na mechi yake ya kwanza akafunga goli vs Liverpool kisha akafunga mawili vs Soton  wiki moja baadae, ilionekana kama hatimaye Van Gaal ameongeza mtu wa maana katika safu yake ushambuliaji. 

Badala yake sasa, mshambuliaji huyo makeke wa kifaransa amepunguzwa kasi kwa kupelekwa kucheza kwenye nafasi ya winga kulingana na mahitaji ya kitu kinachoitwa “philosophy” – huku Mdachi huyo akitumia viungo wawili wa kukaba kama tulivyoona vs Leicester akiwapanga Michael Carrick and Bastian Schweinsteiger.

Viungo hao wote wawili ni wazito, ingawa mjerumani Bastian alifunga magoli mawili vs Leicester na Watford – lakini mara nyingi amekuwa akicheza nyuma zaidi. 

United, walikuwa wakicheza taratibu mno na kuboa vs PSV wiki iliyopita, na hali hiyo ikazidi zaidi kwenye mechi vs Leicester. Wote walionekana timu za kawaida.  

  
Juan Mata alicheza namba 10  lakini hili halikutibu ugonjwa wa United kutokuwa na kasi  – na wakati nguvu na kiwango cha Wayne Rooney kizidi kushuka, United imekuwa ikikosa kasi na mashambulizi ya nguvu kama ambavyo mashabiki wa klabu hii walivyokuwa wamezoea. 

Van Gaal alilamika kwa timu yake kushindwa kupata ushindi jumamosi, akazungumzia namna walivyoitawa mechi – lakini alikuwa anaongea vitu ambavyo havina msingi ambayo vilikuwa vinapingana na ukweli. 

Kwa ushahidi wa msimu huu tu, Inaonekana Van Gaal anataka timu yake kwa kufuata mfumo wake usioruhusu uchezaji mwingine nje ya mfumo elekezi – jambo ambalo linazorotesha matumizi ya vipaji binafsi, mfumo wa timu unatokana na marudio ya mazoezi wanayofanya kwenye dimba la mazoezi.

Rekodi yao nzuri ya safu ya ulinzi ambayo imeruhusu magoli  10 tu, idadi ndogo zaidi kwenye ligi, hili linatokana na timu kucheza kwa kuzuia zaidi, tofauti na mategemeo ya mashabiki. 

Mpaka ilipofika dakika ya 74 vikaanza kusika vilio vya mashabiki waliosafiri na timu “attack, attack, attack”. 

Hata hivyo itawabidi kusubiri kwa kuda kuona kama kama watapata wanachotegemea kwa sababu ni wazi kikosi hiki hakijajengwa kutimiza matakwa yao. 

Je Mashabiki wa Man United wapo sahihi kulalamikia uchezaji wa timu? 

  Jarida linaloheshimika la Red Devils fanzine United We Stand hivi karibuni liliandika habari iliyobeba kichwa cha habari hiki: “It’s Not What You Do It’s The Way That You Do It”(Haijalishi nini Unafanya, Ni Namna Gani Unafanya). Hii ilikuwa baada ya sare dhidi ya PSV katika  Champions League Jumatano iliyopita- hali ilikuwa mbaya mpaka baadhi wasikilizaji wa BBC Radio 5 waliomba Moyes arudishwe..
Jumamosi baada ya mechi ya ligi – wengine walitweet na kuandika hata kama ikitokea United wakashinda EPL haitokuwa jambo la kufurahisha sana au lenye kukumbukwa. 

Ukiangalia msimamo wa ligi pekee mashabiki hawana haja ya kulalama lakini ukiangalia aina ya uchezaji wa timu basi wanayo haki ya kulalama. 

Ikiwa United watashinda ubingwa or Van Gaal akileta ubingwa mwingine wowote, atakuwa kajibu wanaoponda utawala wake katika namna nzuri zaidi.  


Tatizo anakabiriwa na uzito wa mafanikio yaliyopatikana chini ya Ferguson – wazungu wanasema standars  have been set highest of all by Ferguson’s reign.

Hata hivyo  huyi ni mtu aliyekuja baada ya kuondoka kwa kocha aliyembadili Fergie, ipo imani kwamba anaweza kuwa ndio mtu atakayerejesha ushindi ‘Theatre of Dreams’. Wazungu wanasema – ‘The wait continues.

Baadhi wanaweza kuona malalamiko ya mashabiki wa United yanatokana na walivyozoeshwa kupata mafanikio huko nyuma. Japo hilo lina ukweli ndani yake lakini pia wanasukumwa na matamanio ya angalai kuona mfanano wa soka waliloliona miaka kadhaa iliyopita – ukizingatia matumizi makubwa ya fedha kwenye usajili. 

Walipata matumaini walipowasili Martial na Depay kwa ada ya jumla ya £67m, lakini furaha ilikatishwa na kuanza vibaya kwa Depay huku Martial akianza kupungua makali. 

Van Gaal anaweza na ataweza kustopisha malalamiko ya mashabiki wa United kwa makombe – lakini aina ya mchezo ulionyeshwa siku ya jumamosi dhidi ya Leicester, na mawazo ya Van Gaal juu ya kutawala mpira hayasadii kupunguza kelele za mashabiki. 

  
Je Man Utd hii inayoboa itaweza kutwaa taji? 

Wanaweza kabisa – lakini itawabidi waombe sana na kutegemea kufeli kwa timu nyingine kuliko kutegemea uwezo wao kwa sababu wanaonekana wamejipanga vyema lakini kuna kitu wanakosa ambacho timu ambazo zinataka ubingwa wanakuwa nacho. 

Mabingwa hawahitaki kucheza kwa kiwango cha juu kila wiki na ubingwa wa wa EPL utapima kila aina ya mbinu ambayo Van Gaal atatumia, lakini kikosi hiki cha Van Gaal hakionekani kama kitashinda ubingwa huu. 

United wamepoteza mechi 2 tu kati ya 14 msimu huu na walikuwa wanahitaji goli moja tu wiki iliyopita kukwea kileleni, hivyo wakiongeza juhudi na mbinu za LVG zikakaa vyema wanaweza kutoka na kitu

MUDA UTAONGEA


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>