Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

MNYAMA SIMBA KESHO MAWINDONI ZANZIBAR

$
0
0
Wachezaji wa Simba SC wakiwa mazoezi kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar
Wachezaji wa Simba SC wakiwa mazoezi kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar

Na Abubakar Kisandu, Zanzibar

Wekundu wa Msimbazi Simba kesho wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kimbunga ambayo inashiriki ligi kuu soka visiwani Zanzibar, mchezo ambao utasukumwa saa 10:00 za jioni kwenye dimba la Amaan.

Katika mchezo huo Simba watautumia kama ni mchezo wa kupata mazoezi na kuwaangalia wachezaji wao wanaotarajia kuwasajili katika dirisha hili dogo la usajili.

Mtandao huu tumefanikiwa kuzungumza na Abdul Mshangama ambae yeye ni mjumbe wa kamati tendaji ya timu hiyo akiwakilisha hapa Zanzibar na kusema kuwa watacheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kuwavaa Azam siku ya Jumamosi ya tarehe 12 ya mwezi huu kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

“Kesho sisi Simba tutacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kimbunga, na pia mchezo mwingine tutacheza na kombaini ya Unguja siku ya Jumamosi, mechi hizi tutazitumia kuwaangalia wachezaji ambao tunatarajia kuwasajili”, amesema Mshangama.

Wakati wakijiandaa na msimu mpya Simba walipokuja Zanzibar walishinda michezo yao ya kirafiki yote kwa kuifunga kombain ya Zanzibar 2-1, pia wakaitwangwa Black Sailors 4-0, na michezo mingine wakaichapa Polisi 2-0,  wakaifunga Jang’ombe Boys 3-0, wakaipiga KMKM 3-2 na kutoka sare ya 0-0 na KVZ,  hivyo wanahistoria nzuri kwa michezo ya kirafiki hapa visiwani kwa mwaka huu.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>