Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

DAUDA TV: NI NANI WA KUIZUIA BARCA? YAFANYA BALAA JINGINE COPA DEL REY

$
0
0

Alves

Ni nani wa kuzuia gharika hii? Miamba ya Hispania na Ulaya timu ya Barcelona usiku wa December 2 iliendeleza wimbi la vipigo kwa kila anayekatiza mbele yao, jana usiku ilikuwa ni zamu ya Villanovense baada ya kuwaporomoshea rundo la magoli 6-1 kwenye mchezo wa Copa del Rey uliochezwa kwenye uwanja wa Nou Camp uwanja wa nyumbani wa Barcelona.

Dani Alves ndiye aliyeanza kufungua mvua ya magoli kwa Villanovense akifunga goli la kwanza dakika ya 4, kisha Sandro Ramirez akafunga dakika ya 21, 31 na 69 wakati Munir El Haddadi akimalizia ushindi kwa magoli yake mawili ya  dakika ya 51 na 76.

Alves 2

Ushindi huo umekuwa ni mwenelezo wa vipigo vizito ambavyo Barcelona imekuwa ikivitoa katika michezo yake ya hivi karibuni, vipigo vya aina hii vilianzia kwenye mchezo wa La Liga baada ya kutoa dozi ya magoli 4-0 dhidi ya Madrid, kisha UEFA Champions League AS Roma ikalala kwa magoli 6-1 halafu wakafuata Real Sociedad wakapigwa 4-0.

Goli pekee la wageni lilifungwa na Juanfran dakika ya 29 na mchezo huo kumalizika kwa Barcelona kuibuka na ushindi mnono wa magoli 6-1.

Alves 1

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>