Wiki chache zilizopita ilibidi wakala huyu afanye makeke ili mkataba usainiwe na De Gea ajiunge na Real Madrid. Lakini kutokana na kile ambacho hakuna hata club moja inakubali ni kosa lake, hadi sasa De Gea ni mchezaji wa Manchester united na uhamisho ulifeli.
Chochote kilichotokea sio kosa la mchezaji, De Gea inabidi aendelee kucheza kama kawaida. Sasa hivi wakala huyu yupo Manchester na amepigwa picha akiwa karibu kabisa na viwanja vya Manchester united kwa ajili ya kukamilisha mkataba mpya wa De Gea na Manchester United.
Ripoti zinasema kwamba kila kitu kimeshajulikana,mchezaji na timu wamesharidhiana kwa ajili ya mkataba huo. Muda wowote wanaweza kudondoka wino kwenye makaratasi na maisha ndani ya jezi nyekundu yakaendelea.