Kama unakumbuka kwenye mechi ya Man City dhidi ya Man United mwaka 2013 ambapo United ilichapwa 2-1 kulitokea crash kati ya Yaya na Rio. Kwenye mchezo huo hadi Ferdinand alionyesha alama ya kidole kikifunga mdomo kwa maana ya kwamba Yaya anyamaze.
Lakini hayo yote yalikua ni sehemu ya mchezo, watu wazima hao wameyamaliza na hivi sasa wapo kazini ambapo Toure bado anacheza na Rio yupo kama mtangazaji wa TV. Kazi yake mpya ya utangazaji ndio imemfanya Rio akutane na Yaya ambapo alikua anamfanyia interview na kama kawaida alipiga picha na kui-post instagram na kusema kwamba “Tulikua na mapambano kidogo na huyu mshkaji……Interview”.
Lakini inasemakana kwamba wamefanya hiyo interview bila tatizo lolote na kila mtu ameendelea na mambo yake bila tatizo lolote.