Mchezaji bora mara nne wa dunia, mu-argentina Lionel Messi amemuelezea Wayne Rooney kuwa ni moja kati ya wachezaji bora zaidi katika kizazi chao. Huku akisisitiza Rooney huweka maslahi ya timu na ushindi mbele zaidi ya chochote.
Akizungumza hivi karibuni mara baada ya Rooney kuweka rekodi ya mabao na timu ya taifa ya England, Messi amesema Rooney ni moja kati ya wachezaji adimu amewahi kukutana nao na kwamba ana uwezo na kipaji na kwamba ni moja kati ya wachezaji bora wa kizazi hiki.
Rooney amefikisha magoli 50 katika timu ya taifa huku Messi akiwa na 49 wakati Ronaldo akiwa na magoli 55, amepokea sifa lukuki toka kwa malegendari na wachezaji wenzake wa soka kutokana na kudumu kwa kiwango chake katika soka.
Messi anasema kitu cha upekee kwa Rooney ni uwezo wake wa kujali zaidi mechi kuliko mambo yake binafsi huku pia akimtaja kama mchezaji asiye mbinafsi anapokuwa uwanjani.
Wakati huo huo mtoto wa Wayne Rooney, Kai(5) alikutana na wachezaji nyota wa Barcelona akiwepo Messi na Neymar na kupiga picha za kumbukumbu huku mtoto huyo akionekana kufurahia kutokana na kumkubali zaidi Lionel Messi.