Hali si shwari katika kikosi cha Manchester United, wachezaji wana mengi moyoni mwao, kocha Louis Van Gaal hana sifa za kuwa baba wala mlezi, Victor Valdes, Rafael ni baadhi ya wachache waliopata wakati mgumu chini ya mzee huyu ‘arrogant’ kama anavyofahamika.
Inaelezwa kuwa mara baada ya mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspur waliposhinda goli 1-0, nahodha Wayne Rooney na Michael Carrick walimfuata Van Gaal kumueleza malalamiko ya wachezaji wengi kuhusiana na treatments zake za kikoloni.
Hata hivyo hakuna kilichobadilika, Van Gaal anaamini katika philosophy zake, wachezaji wanaumia, hawainjoi hata kidogo. David de Gea ni muathirika wa hivi karibuni, huku kambi nzima ya Manchester United ikiwa haifurahii maisha Old Trafford.
Kocha huyo kaweka sheria na ratiba nyingi za kuwabana sana wachezaji, zisizo na mashiko ambapo wachezaji hulazimishwa kula pamoja, huku kukiwa na vikao lukuki kabla na baada ya kila mechi kitu kinachowanyima uhuru wachezaji kufurahia soka yao.
Wachezaji wanajikuta watumwa chini ya Van Gaal, hawasikilizwi.. hawana amani, wanafuatiliwa katika kila sekunde ya maisha yao Old Trafford, wanachoka, hawana la kufanya.
Van Gaal wiki iliyopita alibwatukiana na mlinzi Marcos Rojo kwa kile Rojo alicholalamika kutotendewa haki kwa kutopangwa katika mechi huku Van Gaal akidanganya umma kwamba Rojo ni mgonjwa, huku stori za Victor Valdes na Rafael da Silva tukiwa tunazijua.
Mambo hayako sawa sana hapa, Giggs amekuwa na msimamo tofauti na Van Gaal na huenda yakaibuka mengi mara baada ya Van Gaal kufungishwa virago Old Trafford, tusubiri kuona.