Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

ISHU YA MAJABVI WA SIMBA SASA IMEFIKA PABAYA…UONGOZI UMESEMA LITAKALOKUA NA LIWE

$
0
0
Kiungo wa Simba SC Justice Majabvi
Kiungo wa Simba SC Justice Majabvi

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kiungo wao wa kimataifa wa Zimbabwe Justice Majabvi kama anataka kuondoka kwenye klabu hiyo ni ruksa kufanya hivyo kutokana na mgogoro uliopo kati ya uongozi na nyota huyo wa nafasi ya ukabaji kwenye kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC Zacharia Hans Poppe amesema hata kama kuna vitu hawajatimiza kwa mchezaji huyo, hatakiwi kwenda kuzungumza nje ya klabu kwasababu mkataba wake unamzuia yeye kwenda kuzungumza nje na kama anafikiri atasaidiwa na vyombo vya habari basi aende akadai hakai yake huko.

“Aende zake tu kwani tunatabu gani sisi. Kama kuna vitu tumetimiza au hatujatimiza hatakiwi kwenda kuanza kupayuka maneno hadharani na mkataba unamnyima yeye nafasi ya kwenda kuzungumza na vyombo vya hari, yeye kama anafikiri atasaidiwa na vyombo vya habari basi aende akadai huko”, amesema Hans Poppe boss wa usajili wa klabu ya Simba.

“Sisi tunasajili mchezaji na kama haki zake hazijatimizwa basi zitashughulikiwa kwahiyo yeye asijifanye mzungu sana, amepewa nyumba tatu anakataa anataka nyumba ya pekeyake akae yeye na familia yake. Mkataba hausemi hivyo, mkataba unasema tutampatia accommodation tumempatia kila nyumba anakataa mpaka mwisho wake tumemuweka hotelini”.

Hans Poppe amesema wao hawataki kusumbuliwa vichwa na mchezaji yeyote siyo yeye tu na kama akitaka kuondoka wao wako tayari kwa hilo.

Majabvi hajasafiri na kikosi cha Simba kilichoelekea Mwanza kucheza dhidi ya Toto Africans kwa madai kwamba haridhishwi na namna kikosi hicho kinavyoendeshwa na inatajwa kuwa kuna matatizo ya ndani kwa ndani kati ya uongozi wa Simba na mchezaji huyo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>