Dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya Ulaya litafunguliwa mwezi January, 2016 kwa ajili ya vilabu kufanya maboresho ya vikosi vyao ili kuendelea na mikikimikiki ya ligi pamoja na michuano mingine. Lakini tayari baadhi ya vilabu vimeshaanza kuanika ni wachezaji gani vinawataka katika kipindi hicho.
Suala la makocha nalo limekuwa likitajwa kwa baadhi ya timu ambazo zinaona makocha wao wameshindwa kufanya vizuri kwenye timu wanazozifundisha na kuanza kuweka wazi ni makocha gani watarithi mikoba yao mara baada ya wao kufunguliwa mlango wa kutokea.
5. Djilobodji kupelekwa Marseille kwa mkopo
Mchezaji wa Chelsea ambaye amecheza kwa kiwango kibovu kwenye klabu hiyo Papy Djilobodji ataondolewa Stamford Bridge wakati wa dirisha dogo la usajili wa mwezi January. Wababe wa ligue 1 Olympique Marseille wanatajwa watamchukua mchezaji huyo kwa mkopo ili kuboresha kiwango chake hadi mwisho mwa msimu. (Source: Mercato365)
4. Chelsea kumsajili Pelle
Inaripotiwa boss wa Chelsea Jose Mourinho anamtaka striker wa Southampton Graziano Pelle 30, mapema wakati wa usajili wa mwezi January ili kuisaidia timu yake ambayo inapambana kutokana na kushindwa kufunga magoli. (CalcioNews24, in Italian)
3. Manchester City imeandaa dau nono kwa ajili ya Guardiola
Taarifa zinasema kuwa, klabu ya Manchester City iko tayari kumlipa kiasi cha pauni milioni 15 kwa mwaka kocha Pep Guardiola ambaye ndiyo top target wao ili kumuweka kocha huyo mbali na mahasimu wao Manchester United. (Daily Mail)
2. Hiddink kuchukua mikoba ya Mourinho
Kocha wa zamani wa Uholanzi na Urusi Guus Hiddink anaripotiwa kuwa ndiye kocha anayepewa nafasi kubwa ya kumrithi Jose Mourinho ambaye amekalia kuti kavu kwenye klabu ya Chelsea.
Kwa mujibu wa ripoti za uhakika, Carlo Ancelotti, kocha wa Atletico Madrid pia wanatazamwa kama makocha ambao wanaweza kupewa mkataba wa kudumu wa muda mrefu lakini hiyo itakuwa ni katika majira ya kiangazi. (Daily Telegraph)
1. Manchester Unided yamtaka Lewandowski
Inaelezwa kwamba, Manchester United iko tayari kulipiku dili la PSG na kumsajili striker wa Bayern Munich Robert Lewandowski kwa kumpa offer ya pauni milioni 15 kwa mwaka. Mabingwa wa Ufaransa pia wako tayari kulipa kiasi kama hicho kwa ajili ya mpolandi huyo kwenye usajili wa majira yajayo ya kipindi cha kiangazi.