
Baada ya afisa habari wa Yanga Jerry Muro kumtupia kijembe afisa habari wa Simba Haji Manara akihoji kuhusu elimu yake huku yeye akitamba kuwa anamaisha bora kuliko mwenzie, Manara ameibuka na kujibu mapigo ya Jerry Muro .
Manara amesema yeye anajivunia kuishi Kariakoo kwasababu ndiyo kwao na ndiyo sehemu ambapo amezaliwa huku akisema hawezi kujibu matusi ya Muro. Manara ameongea kuwa yeye alitoa hoja na hoja yake haikujibiwa badala yake msemaji wa Yanga amekuwa akijisifu na kujitapa kuhusu kuishi sehemu nzuri na kutembelea gari zuri.
Angalia hii video inayomuonesha Haji Manara akifunguka kuhusu Jerry Muro.