Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

AFRICAN SPORTS VS SIMBA, JE WEKUNDU WA MSIMBAZI WATAVUNJA MWIKO MKWAKWANI?

$
0
0
Kikosi cha Simba kilichocheza dhidi ya Sports Club Villa siku ya 'Simba Day'

Kikosi cha Simba kilichocheza dhidi ya Sports Club Villa siku ya ‘Simba Day’

Mchezo wa ligi kuu kati ya African Sports ya Tanga dhidi ya Simba SC yajijini Dar es Salaam ni kati ya mihezo ambayo inatazamwa kwa jicho la tatu ikiwa leo ndio pazia la ligi kuu Tanzania bara (VPL) msimu wa 2015/16 linafunguliwa na kupigwa kwa michezo saba. Timu hizi zinatofautiana kwa mambo mengi, lakini hapa kuna baadhi ya vitu muhimu ambavyo utapata kujua kati ya timu hizo kabla ya mchezo wao kupigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Usajili wa timu hizo mbili

African Sports

Wamepanda daraja msimu huu baada yakusubiri kwa miaka 23 watakuwa na kibarua kigumu kutokana na ukweli kwamba hawajafanya usajili wa wachezaji wengi wenye majina makubwa zaidi ya Nsa Job na Zahoro Pazzi.

Simba

Wamefanya usajili wa wachezaji wa kitaifa na kimataifa, wamewarejesha wachezaji wao wa zamani Mussa Hassan Mgosi na Mwinyi Kazimoto, wamemsajili Peter Mwalyanzi, Hamisi Kiiza, hawa wote wanauzoefu na ligi kuu Tanzania bara. Lakini Simba hawajaishia hapo, wamesajili wachezaji wengine wengi kama golikipa, viungo na washambuliaji wa kimataifa ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye ligi.

Kiu ya timu zote

African Sports

Wanataka kuonesha kwamba walikuwepo kwenye ligi tangu enzi hizo na kwamba sio wageni kwenye ligi na wanajua wanachokifanya. Wakati huohuo watakuwa wakitaka kuweka historia ya kuifunga timu yenye jina kubwa kwenye mchezo wao wa kwanza mara baada ya kupanda kucheza ligi kuu.

Simba

Inataka kuvunja historia ya kushindwa kuondoka na pointi tatu kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Simba imepata ushindi kwa mara ya mwisho kwenye uwanja wa Mkwkwani mwaka 2011. Baada ya hapo utawala wake ukapotea kwenye uwanja huo kutokana na vipigo kutoka kwa Mgambo JKT na Coastal Union na ikitokea wamepata ushindi basi ni sare.

Uzoefu wachezaji wa timu zote kwenye ligi kuu

Simba

Inawachezaji wengi ambao wameizoea ligi wanajua ligi inataka nini, hii inaweza kuwa changamoto kubwa sana kwa wachezaji wa African Sports kuwazuia wachezaji wa Simba ambapo pia inawachezaji wengi wa kulipwa tofauti na ilivyo kwa African Sports.

African Sports

Asilimia kubwa ya wachezaji wa kikosi cha African Sports ni wale ambao wameipandisha daraja timu hiyo huku waliosajiliwa wakiwa ni vijana wasio na majina wala uzoefu kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi

Simba

Imekuwa na maandalizi mazuri ukilinganisha na wapinzani wao, Simba iliweka kambi yake ya kwanza Lushoto kwa muda wa wiki mbili, baada ya hapo ikaenda Zanzibar ikajifua na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na kufanya vizuri. Ikarejea Dar es Salaam kwa ajili ya siku ya Simba ‘Simba Day’ ambapo walicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya SC Villa ya Uganda na kuibuka na ushindi. Baadae ikacheza na URA ya Uganda pia. Baadae Simba ikarejea tena visiwani Zanzibar kujiandaa na michuano ya ligi.

African Sports

Timu hii haikuwa na maandalizi ya kutisha kuelekea msimu wao wa kwanza kwenye ligi kuu baada ya miaka 23. Haikupata fursa ya kucheza michezo mingi ya kirafiki dhidi ya timu ngumu mbali na Azam FC na Coasta Union.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 9000

Trending Articles