Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea kujifua kwenye uwanja wa chuo cha DIT jijini Mwanza kuelekea kwenye mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa December 26 siku ya Boxing Day.
Simba itachuana na Mwadui kwenye uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga ikiwa ni baada ya kubanwa kwenye mchezo wao uliopita walipokutana na Toto Africans ya Mwanza.
Kuelekea mchezo huo, Simba inakumbukukumbu mbaya kwani imetoa sare kwenye mechi mbili mfululizo wakati Mwadui FC yenyewe imeshinda michezo yake yote miwili iliyopita. Simba ilitoka sare dhidi ya Azam FC kwa kufungana bao 2-2 kwenye uwanja wa taifa, kisha ikatoka sare ya kufungana kwa goli 1-1 na Toto Africans.
Mwadui yenyewe ilishinda kwa bao 2-0 dhidi ya Stand United kabla ya kupata ushindi mwingine wa goli 2-1 ilipocheza dhidi ya Ndanda FC.
Simba inaweza ikawa na faida ya kumtumia kiungo wake mzimbabwe Justice Mabvi ambaye amejiunga na timu hiyo baada ya kugoma kusafiri na timu kufuatia matatizo kati ya uongozi na mchezaji huyo.
PICHA ZAIDI