
Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima amekuwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo vya habari nchini kwa siku kadhaa sasa baada ya uongozi wa klabu yake kumsimamisha kwa muda usiojulikana pamoja na kumlipa nusu mshahara kwa muda wote ambao atakuwa amesimamishwa kukitumikia kikosi cha Jangwani.
Jana katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha alizungumza na mtandao huu na kuweka wazi baadhi ya mambo ambayo wadau wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu sakata la mchezaji huyo lakini pia kamati ilitakiwa kukutana ili kujadili mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kupitia utetezi wa Niyonzima.
Dkt. Tiboroha amefafanua chimbuko au chanzo cha mchezaji huyo kusimamishwa na klabu yake na hatuanyingine ambazo zitafuta.
“Chimbuko lake ni issue ya kawaida tu klabu inahitaji uwepo wa mchezaji kwenye program za timu anapohitajika kuondoka kwenda kwenye shughuli zake za timu ya taifa kwa ruhusa lakini pia kurudi kutoka kwenye majukumu ya taifa kwa muda unaotakiwa kwasababu haya masuala si ya Yanga tu lakini ni ya kikanuni za FIFA, kwamba kama ni mechi za qualifying mchezaji anatakiwa afike kabla ya masaa 48 na baada ya kuitumikia timu yake ya taifa masaa 48 baadae anatakiwa arudi kwenye klabu yake”, alisema Dkt Tiboroha.
“Sasa inapotokea mchezaji hayupo kwenye timu kwasababu alikuwa kwenye timu yake ya taifa halafu anakosa mechi za kwenye ratiba ya ligi hicho kitendo tumeona hatuwezi kuendelea kukivumilia lazima tujue sababu yake ni nini lazima tupate maelezo ya kina kutoka kwa mchezaji atuambie nini sababu ambayo imekuwa ianasababisha achelewe kurudi”.
“Tumekaa na mchezaji tumeongea ameona kwanini klabu inataka kujua hilo na kwa ujumla wake amekubaliana na mambo mengi ambayo klabu imelalamika kuhusu hicho kitu na tumemuomba aandike ili tuweze kutafuta suluhisho la mambo haya ili tujue tutafanya kitu gani”.
Hapa unaweza kumsikiliza Dr. Tiboroha akipiga story na Shaffih Dauda huhusu issue ya Haruna Niyonzima.