Quantcast
Channel: ShaffihDauda
Viewing all 9000 articles
Browse latest View live

Nizar atoa tahadhari VPL 2017/18

$
0
0

Nahodha wa Singida United Nizar Khalfani amewaambia wapenzi wa timu hiyo kuipa sapoti timu yao kutokana na mipango ya kufanya makubwa kwenye msimu ujao. Nizar amesema wamepanga kufanya mapinduzi makubwa kwenye soka la Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.

“Tumejipanga kufanya mabadiliko kidogo kwa sababu ukiangalia timu zinazopanda mara nyingi zinashuka lakini kwetu sisi tunataka iwe tofauti.”

“Ukiangalia usajili tulioufanya na tulivyojipanga, wao wenyewe wameona timu ina malengo makubwa. Malengo yetu ni kuchukua ubingwa ndio maana wamevutiwa na kuona kuna kitu ambacho tutakifanya kitawanufaisha hata wao.”

“Tunataka tuwe kama Leicester City walivyopanda daraja na kuchukua ubingwa wa ligi na tumekuja kupambana hadi mwisho.”

Singida United imerejea tena kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya kuwa nje ya ligi kwa muda mrefu tangu iliposhuka hakukuwa na timu nyingine ya mkoa huo iliyoshiriki VPL.


Video: Manula kumfuata Bocco Simba?

$
0
0

Wakati John Bocco akihusishwa kujiunga na klabu ya Simba baada ya kumaliza mkataba wake Azam kumekuwa na story nyingi zikiwahusu wachezaji wengine wa Azam (Aishi Manula na Shomari Kapombe) wakitajwa kutakiwa na wekundu wa Msimbazi.

Dauda TV ilimnasa Manula kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za VPL 2016/17 na kupiga nae story kuhusu kuhusishwa kujiunga na Simba lakini akasema hizo ni tetesi, yeye bado ana mkataba na Azam na yupo kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ili kuongeza mkataba mpya kuendelea kuhudumu Azam FC.

“Hizo ni tetesi zinavuma lakini mimi bado nipo Azam japo mkataba wangu unaelekea ukingoni lakini naamini bado nitaendelea na Azam na tumeshaanza mazungumzo kwa ajili ya mkataba mpya,” alisema Manula.

Wakati huohuo, afisa habari wa Azam FC Jafari Idd amethibitisha kwamba, klabu ya Azam imeachana na Bocco baada ya mkataba wa mkongwe huyo kumalizika.

“John Bocco mkataba wake umekwisha kwa mujibu wa bodi ya Azam na uongozi hautaendelea na Bocco kwa hiyo anakuwa ni mchezaji huru, hivyo anauhuru wa kuamua aende wapi ndani au nje ya nchi.”

“Sisi kama Azam klabu tunamtakia kila la heri anapokwenda, ameitumikia timu kwa muda mrefu na kuwa seheu ya mafanikio ya timu tangu wakati timu ikiwa inapambana kupanda daraja mpaka tunakwenda kucheza michuano ya kimataifa kwa hiyo hatutamsahau  kwa mchango wake.”

“Lolote linalomhusu Bocco kwa sasa ni vizuri akatafutwa mwenyewe anaweza kueleza yuko wapi au anakwenda wapi kwa sababu ni maamuzi yake mwenyewe.”

Idd pia akazungumzia hali ilivyo kuhusu Manula na Kapombe kama wataendelea kuwepo Azam au wataondoka kama ambavyo taarifa zinazidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Manula na Kapombe haijamalizika kama ilivyo kwa Bocco , wao bado wana muda wa kubakia Azam kwa mujibu wa mikataba yao. Hadi sasa uongozi bado haujaniambia kuhusu hilokwa hiyo siwezi kutangaza mkataba wamtu umebaki muda gani kwa sababu ni siri kati ya mchezaji na waajiri wake.”

“Hadi sasa ni Bocco hakuna mtu mwingine ambaye tumempa barua ya mkono wa kwaheri.”

Video: Kuelekea fainali ya FA Cup, jezi za Yanga zaiteka Dodoma

$
0
0

Kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba na Mbao FC, kumetokea jambo ambalo linashangaza lakini ndivyo ilivyo na maisha yanasonga hapa mjini Dodoma.

Licha ya game hiyo kuzihusisha Simba na Mbao, ukipita kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma unakuta jezi kedekede za Simba na Yanga zikiwa zinaunzwa na mashabiki wengine wakiwa wametipigilia tayari.

Dauda TV ikaona isiwe kesi, ikazungumza na mfanyabiashara wa jezi hizo ili kujua ni kwa nini kuna jezi kibao za Yanga wanaziuza ikiwa timu hiyo haihusiki kabisa kwenye mchezo unaotarajiwa Mei 27, 2017.

Jamaa akasema popote pale Yanga Tanzania Yanga ikicheza mpinzani wake anakuwa Simba na Simba pia wakicheza Yanga wanakuwa wapinzani wao, kuhusu kutouza jezi za Mbao jamaa analalamika kuwa hazina soko na ukiwa nazo zitakudodea.

Story zaidi unaweza kuiangalia hapa chini kwenye Dauda TV ili ushuhudie mwenyewe jamaa anavyo fafanua kwa nini wanazipiga chini jezi za timu ambazo hazina majina.

Licha ya Mbao kuitoa Yanga katika mchezo wa nusu fainali wa mashindano ya FA Cup, mashabiki wa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara wanatarajiwa kuipa sapoti Mbao lakini si kuishangilia Simba ambao ndio mahasimu wakubwa.

Video: Uchambuzi wa Shaffih Dauda kuelekea fainali ya FA Cup Simba vs Mbao

$
0
0

Saa chache kabla ya kupigwa game ya fainali ya Azam Sports Federation Cup (FA Cup) Dauda TV inakuletea uchambuzi kwa ufupi kuhusu mechi hiyo itakayochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Shaffih Dauda ameeleza mambo kadha wa kadha kuhusu timu hizo zilivyo na njaa ya kushiriki michuano ya Afrika kwa ngazi ya vilabu. Simba ilivyosota miaka kibao kupigania kurudi kwenye anga za kimataifa baada ya kuwa nje kwa muda mrefu, Mbao wanataka kufanya mapinduzi na kuweka historia kwenye soka la bongo kwa kutoka ligi daraja la kwanza na msimu huohuo kwenda michuano ya kimataifa.

Unaweza kuangalia uchambuzi wote wa Shaffih Dauda kupitia video hapo chini na kutoa maoni yako kwa ku-comment wewe unamtazamo gani juu ya mechi hiyo ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hii itachezwa nje ya Dar.

Manchester United watawala kikosi bora cha Europa.

$
0
0

Baada ya michuano ya soka ya Europa kumalizika hatimaye shirikisho la soka UEFA limetoa orodha ya majina ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano hayo ambayo bingwa aliibuka Manchester United.

Katika kikosi hicho golikipa namba moja ni mlinda mlango wa Celta Vigo Sergio Alvarez akisaidiwa na golikipa wa mabingwa wapya wa michuano hiyo Sergio Romero.

Katika nafasi ya ulinzi, kati ya walinzi sita walioko katika kikosi hicho kuna walinzi watatu kutoka katika kikosi cha Manchester United ambao ni Eric Bailly,Daley Blind na Antonio Valencia, wengine ni Jeremy Morel wa Lyon, Gustavo Cabral wa Celta Vigo na Mathhijis Ligt wa Ajax.

Katika nafasi ya kiungo Ander Herrera, Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan wa Manchester United wamefanikiwa kuingia katika tuzo hizi na wengine ni Pablo Hernandez wa Celta Vigo, Corentin Tolisso wa Lyon, Amini Younes wa Ajax na Youri Tielemans wa Anderchelt.

Washambuliaji ni Zlatan Ibrahimovich wa Manchester United, Alexandre Lacazatte wa Olympique Lyon na Bertand Troure wa klabu ya Ajax ya nchini Uholanzi.

 

Lukaku kucheza dhidi ya Abdi Banda na Kelvin Yondani.

$
0
0

Sasa ni wakati wa timu kujiandaa kwa ajili ya msimu wa ligi wa mwaka 2016/2017, hii ni baada ya ligi kuu takribani zote kuwa zimeshamaliza ligi katika mataifa yao.

Jambola kutia moyo na kusisimu ni kwamba klabu ya Everton imetoa taarifa rasmi kwamba katikati ya mwezi ujao watakuwa klabu ya kwanza EPL kuja Africa Mashariki.

Wakiongozwa na mshambuliaji wao hatari Romelu Lukaku Everton watafika katika ukanda wetu wa Afrika na kati ya nchi zitakazotembelewa ni nchi yetu ya Tanzania.

Hii ina maana vilabu vyetu vitapata nafasi ya kujipima nguvu dhidi ya klabu hiyo,Yanga na Simba wanaweza kupata nafasi kucheza na timu hiyo kongwe toka nchini Uingereza.

Tayari kupitia ukurasa wao wa Twitter, klabu hiyo imetoa taarifa rasmi kwamba katika maandalizi ya msimu ujao wa ligi watakuja katika ukanda wa Afrika Mashariki kujiweka sawa.

Katika msimu uliomalizika wa ligi, klabu ya Everton ilifanikiwa kumaliza katika nafasi ya saba ikiwa ni nafasi moja chini ya mabingwa wa Europa klabu ya Manchester United.

 

Habari kwa mashabiki wa Manchester United.

$
0
0

Baada ya lawama na maneno mengi kuhusu kiungo Paul Pogba sasa kocha wake Jose Mourinho ameibuka na kumtaftia dawa ambayo ana uhakika akiipata itawafanya mashabiki wamshangilie Pogba kila wakati.

Mourinho baada ya kuumizwa kichwa kwa muda mrefu sasa anaona kiungo wa PSG Blaise Matuidi ndio muarobaini wa tatizo na kiwango cha Pogba, Mourinho anataka kumleta Matuidi Old Trafford ili kujaribu kumchezesha pembeni ya Paul Pogba.

Lakini achilia hayo ya Pogba, kuna habari ambazo sio nzuri sana kwa mashabiki wa klabu ya Manchester United kwani klabu ya Barcelona imepiga hodi katika timu hiyo ili kuchukua mchezaji wao muhimu.

Taarifa zinasema klabu ya Barcelona imetuma maombi rasmi katika klabu hiyo ili kuona uwezekano wa kumsajili kiungo wa timu hiyo Ander Herrera ambaye amekuwa na msimu mzuri sana na Manchester United.

Wakati huo huo Pierre Aubemayang ambaye United wanamtaka kwa dau la £40m inasemekana amewaambia mabosi wake wa Borussia Dortmund kwamba anataka kuondoka katika klabu hiyo.

Lakino pia Manchester United hao hao wameanza mchakato wa kumnunua Andrea Belotti kutoka Torino ambapo wanaamini wakimnunua Belotti na Griezman watakuwa na safu bora kabisa ya ushambuliaji.

 

Safishasafisha ya Pep Gurdiola inaendelea.

$
0
0

Tayari Pablo Zabaleta na Jesus Navas wameshaoneshwa mlango wa kutokea Etihad baada ya kocha Pep Gurdiola kutokukubali viwango vya wachezaji hao.

Pep Gurdiola anaonekana kama anataka kuanza upya kwani toka msimu uishe ni wiki moja tu umepita lakini tayari wachezaji wasiopunguwa wanne wameoneshwa mlango wa kutokea Manchester City.

Sasa baada ya Navas na Zabaleta kuonesha pa kuondokea, beki wa kulia wa timu hiyo Bacary Sagna na mlinda mlango wao Willy Caballero nao wameoneshwa mlango wa kutokea.

Sio hao tu kwani Gael Clichy mlinzi wa kulia wa timu hiyo naye ameoneshwa mlango wa kuondokea Man City baada ya klabu hiyo kutoridhishwa na kiwango chake.

Taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu hiyo zimethibitisha kwamba Sagna na Caballero hawatakuwepo Etihad msimu ujao na wanaruhusiwa kuanza kutafuta timu ya kuchezea msimu ujao.

Tetesi zinasema pia mshambuliaji wa klabu hiyo Kun Aguero huenda akaondoka katika klabu hiyo kwani hana furaha na maisha ya klabu hiyo, Aguero muda wake uwanjani umekuwa mdogo tangu Gabriel Jesus ajiunge na klabu hiyo.

 


Rekodi zinawabeba Arsenal kuwafunga Chelsea hii leo.

$
0
0

Sikia hii, hivi unajua kwamba katika mara nane za mwisho Chelsea kukutana na Arsenal katika michuano ya FA klabu ya Chelsea ilifungwa mara saba?

Na je unafahamu kwamba mwaka 2009 wakati Chelsea walipoifunga Arsenal katika michuano hiyo kwa mabao 2 kwa 1 ilikuwa ndio ushindi wao pekee dhidi ya Arsenal ndani ya miaka 70 iliyopita katika michuano hiyo?

Sahau sasa kuhusu yote hayo ila leo huku Antonio Conte na huku ni Arsenal Wenger wataoneshana nani mbabe kati yao katika fainali ya michuano ya FA mchezo unaoenda kupigwa katika dimba la Wembley.

Wakati Chelsea wenyewe wako fiti 100% kuna tatizo haswa katika safubya ulinzi ya Arsenal ambapo Laurent Koscienly ana adhabu, huku Kieran Gibbs na Shkodran Mustafi wakiwa ni majeruhi.

Kama ni rekodi tu baasi Arsenal wanaweza kubebwa na rekodi kwa maana katika mechi zao saba za mwisho katika uwanja wa Wembley hawajawahi kupoteza hata mchezo mmoja.

Chelsea wenyewe hii ni fainali yao ya saba katika michuano hii ya FA katika karne hii na fainali zao nne za mwisho katika michuano hii walishinda zote na wakishinda kwa tofauti ya bao moja kila fainali.

Toka tajiri Roman Abromovich aichukue klabu hii ya Chelsea imepoteza fainali kubwa mbili tu na zote ikiwa ni 2008,moja ilikuwa UEFA champions nyingine ikiwa fainali ya ligi dhidi ya Tottenham.

Lakini pia kocha wa Chelsea Antonio Conte anaingia katika fainali hizi akiwa hana rekodi nzuri kwani fainali yake ya mwisho kubwa kama kocha ilikuwa mwaka 2012 dhidi ya Napoli na Juve wakifa kwa bao 2 kwa 1.

 

Simba wamerejea kimataifa

$
0
0

Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa taji ls Azam Sports Federation Cup (FA Cup) baada ya kuifunga Mbao bao 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ushindi wa Simba umewapa ubingwa wa kombe, pesa kiasi cha shilingi milioni 50 za Tanzania pamoja na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Ilikua ni fainali ya aina yake, soka likapigwa kwa kiwango cha juu na kuburudisha mashabiki walioujaza uwanja wa Jamhuri kushuhudia fainali iliyozikutanisha timu mbili, moja ikitoka Magharibi mwa Tanzania huku nyingine maskani yake yakiwa ni Mashariki.

Dakika 90 zilimalizika timu zote zikiwa hazijafungana na kulazimika kuongezwa dakika 30 za kuendelea kumtafuta bingwa mwa mwaka 2017.

Simba walipata bao lao la kwanza dakika 15 za kwanza za muda wa nyongeza kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Ivory Coast Fredrick  Blagnon.

Mbao walipambana na kusawazisha bao hilo kipindi cha pili cha dakika za nyongeza na kuwaongezea Simba mlima ambapo baadhi ya mashabiki walitumaini mchezo ungemalizika kwa Simba kushinda 1-0.

Kipenzi cha wanamsimbazi Shiza Kichuya akaipa Simba ndoo kwa kuifungia goli kwa mkwaju wa penati kufuatia beki wa Mbao kuushika mpira akiwa kwenye eneo la hatari wakati akifanya harakati za kuokoa.

Penati hiyo ilizua utata baada ya wachezaji wa Mbao kuanza kumzonga mwamuzi wakipinga maamuzi yake hadi askari polisi wakalazimika kuwatuliza wachezaji wa Mbao na kuweka mwamuzi katika hali ya usalama.

Mwigulu Nchemba kaufuata ubingwa Simba?

$
0
0

Hakuna asiyejua kwamba Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba ni shabiki wa Yanga ‘lialia.’

Kamera ya shaffihdauda.co.tz ilifanikiwa kumnasa Nchemba akiwa anaitinga jezi ya ‘mnyama’ Simba kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mh. Nchemba anafahamika kuwa ni mpenzi wa Yanga na mara kadhaa ameonekana akiwa katika uzi wa klabu hiyo na pia amekuwa akionekana kuwa karibu na klabu hiyo kama kuhudhuria mazoezi na kusuluhisha baadhi ya migogoro pale inapotokea mambo hayaendi sawa.

Kabla ya mchezo wa fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba dhidi ya Mbao, ulipigwa mchezo wa utangulizi kati ya Azam Media dhidi ya Bunge FC ambapo Bunge FC walishinda 2-1. Baada ya mchezo huo, Mwigulu alionekana jukwaani akipigilia uzi mwekundu wa Simba wenye jina la Ajibu.

Si kitendo cha kawaida kwa shabiki au mpenzi wa timu hizo mbili kuvaa jezi ya mpinzani wake lakini pia si vibaya kuvaa kuonesha ushabiki na utani wa kweli kati ya timu hizo.

Haikujulikana mara moja kwa nini Mwigulu aliamua kuvaa jezi ya Simba dakika chache kabla ya game ya fainali kuanza kupigwa ambapo mechi ilimalizika kwa Simba kushinda 2-1 na kutwaa ubingwa wa ASFC unaowapa tiketi ya kufuzu kushiriki michuano ya kimataifa ya Afrika.

Mwigulu amekuwa akitumia vizuri ushawishi wake katika kuweka mambo sawa ndani ya klabu ya Yanga, kama unakumbuka ni yeye ndiye alipambana kumshawishi Hans van Pluijm kurejea Yanga mara baada ya kuandika barua ya kujiuzulu aliposia klabu hiyo inamleta George Lwandamina kuchukua nafasi yake bila yeye kujua.

Alionekana pia hotelini akihamasisha wachezaji wa Yanga siku moja kabla ya mchezo wa raundi ya pili kati ya Simba na Yanga na hata wachezaji walipotaka kugoma kucheza kutokana na kutolipwa mishahara, alikua mstari wa mbele kuwashawishi wacheze kwa maslahi ya klabu yao.

Mambo 6 yaliyo bamba fainali ya ASFC uwanja wa Jamhuri Dodoma

$
0
0

Fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya Simba dhidi ya Mbao ilikuwa ni ya kiwango cha juu na ilistahili kuitwa fainali inayotoa mshindi anaekwenda kushiriki michuano ya kimataifa na kuiwakilisha nchi.

Ukiachana na uhondo wa fainali hiyo, kulikuwa na burudani nyingine nje ya uwanja ambapo inawezekana kwa wale ambao hawakuwepo uwanjani iliwapita au hata wale waliokuwepo uwanjani walipitwa kutokana na sehemu walipokuwa wamekaa.

Shaffihdauda.co.tz inakuletea matukio sita yaliyo bamba nje ya uwanja na kuwa kiburudisho kwa wengine .

Farasi

Farasi aliyetumika kupambana na mashabiki waliokuwa sio waungwana wakati wa mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho (Azam Sports Federation Cup) alikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wengine waliokuwa uwanjani wakishuhudia fainali hiyo iliyozikutanisha Simba na Mbao.

Farasi huyo aliyekuwa akiongozwa na askari wa jeshi la polisi alikuwa akikabiliana na mashabiki ambao sio wastaarabu waliokuwa wakitoka kwenye maeneo yao na kushuka chini kwenye maeneo ya kukimbilia.

Mara kadhaa polisi akisaidiwa na Farasi aliwakimbiza mashabiki na kuwapeleka kwa askari wengine ambao walikuwa wanawakamata mashabiki kwa urahisi na kuwaingiza ndani ya magari yao na kupunguza ghasia ambayo ingeweza kutokea na kuharibu mchezo.

Kitendo cha Farasi kupambana na mashabiki wasio wastaarabu kilikuwa ni kivutio kwa mashabiki wengine ambao ni wastaarabu na mara kadhaa walionekana wakishangilia mambo yaliyokuwa yakifanywa na Farasi.

Raia wa kigeni

Kwa mujibu wa takwimu unaambiwa mchezo wa soka ndio mchezo unaoongoza kwa kupendwa ulimwenguni halafu michezo mingine inafuata nyuma.

Mchezo wa soka unakutanisha watu wa rika tofauti, makabila, dini, itikakadi, mataifa na mambo mengine kibao, kwenye mchezo wa fainali ya ASFC, kuna raia wengi wa kigeni walijitokeza kushuhudia mxhezo huo ambapo walikuwa kivutio pia kwa mashabiki waliokuwepo uwanjani kwa sababu walionekana wakishangaa namna ushangiliaji wa wabongo hususan kikundi cha mashabiki wa Mbao waliokuwa wakishangilia kwa style ya aina yake.

Mashabiki wa Mbao

Hawa unaweza kuwafananisha na wale mashabiki wa Sports Extra Ndondo Cup kutokana na ubunifu wao wa hali ya juu kwa kujichora kwao, mavazi, nyimbo na hata mavazi pamoja na kubeba vitu vya asili ya mwafrika mfano kubeba chungu chenye moto kichwani.

Aina yao ya ushangiliaji wa mwanzo mwisho bila kujali timu yao inashambulia au inashambuliwa hata pale ilipokuwa nyuma kwa matokeo wao hawakuacha kushangilia. Walikuwa ni kiburudisho tosha kwa mashabiki wengine waliokuwepo uwanjani kutokana na burudani waliokuwa wanaitoa.

Shabiki wa Simba

Ahazi Sadock Mwembe huyu ni shabiki wa Simba kutoka Tunduma, Songwe. Ubunifu wake aliokuja nao kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma ulikuwa kivutio na kiburudisho tosha ukiachana na mambo mengine ya pembeni.

Kwanza huyu jamaa ametumia ghrama kubwa kutengeneza hivyo vitu unavyomuona navyo, msumeno umegharimu Sh. 25,000 hilo kombe alilobeba kichwani amefinyangiwa kwa 50,000 jamaa hakai kwenye majukwaa ya bei rahisi anakata tiketi za VIP jukwaa la VIP kwenye mchezo wa fainali ya ASFC tiketi zake ziliuzwa 20,000 achana na nauli ya kutoka Tunduma na kurudi, hotel, usafiri wa ndani na mambo mengine.

Kwa hiyo ukimuona shabiki analia baada ya timu yake kupoteza mechi huwa kuna mambo mengi ndani yake mbali na mapenzi kwa timu, ushindi pekee ndio huwa unalipa gharama zote hizo na kumfanya asahau kila kitu.

Ustaarabu wa mashabiki

Utaratibu uliotumiwa na mashabiki wa Dodoma na wengine waliosafiri kutoka maeneo mengine pia ulikuwa kivutio na ulionesha ustaarabu wa mtanzania halisi. Mashabiki walianza kuingia uwanjani kuanzia saa 2:00 asubuhi wakiwa kwenye mistari bila kuambiwa na mtu wala kushurutishwa.

Hakukuwa na kupishana kati ya mashabiki wenyewe wala mashabiki na jeshi la polisi, hakuna shabiki aliyepigwa hata kibao, mashabiki walijiongoza wenyewe na kila mmoja alikuwa mlinzi wa mwingine kuhakikisha utaratibu unafuatwa.

Hiki kitu ni mara chache kukiona katika maeneo mengine ya nchi hususan Dar es Salaam ambapo kila mtu angetaka kuleta ujanja wa kuja kachelewa halafu anataka kuwa wa kwanza kuingia uwanjani na huo ndio huwa mwanzo wa vurumai na poilisi kulazimika kutumia nguvu ya zaida ili kuleta utulivu. Katika hili HONGERENI mashabiki mliojitokeza kushudia mchezo wa fainali ya ASFC kwenye uwanja wa Dodoma.

Breaking: Jonas Mkude wa Simba apata ajali mbaya

$
0
0

Masaa kadhaa baada ya kuiongoza timu yake ya Simba SC kurejea katika anga ya kimataifa kwa ushindi wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mbao FC, kiungo wa Simba Jonas Mkude ameripotiwa kupata ajali mbaya akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.

Nahodha huyo wa Simba amepata ajali hiyo maeneo ya Mitibora, Dumila mkoani Morogoro akiwa njiani kurejea Dar es Salaam kuiwahi Taifa Stars. Taarifa za awali zinasema ameumia maeneo ya shingoni, amekimbizwa kwenye hospitali ya mkoa wa Morogoro pamoja na majeruhi wenzie ambao baadhi wana halimbaya.

Kwenye gari ambayo Mkude amepata nayo ajali walikuwepo watu 6, na kilichopelekea ajali hiyo ni kupasuka kwa tairi la nyuma. Majeruhi mmoja yuko mahututi.

Tutaendelea kujuzana hali yake na majeruhi wengine kadri taarifa zitakavyokuwa zinatoka. 

Hivi unajua?kutapigwa El Classico 3 kabla ya msimu kuanza.

$
0
0

Ni fainali ya Champions League tu ndio imebaki ili kukamilisha michezo yote ya msimu wa 2016/2017 kwani tayari karibia ligi zote kuu zimemalizika.

Lakini jambo la faraja kwa mashabiki wa soka ni kwamba pambano la kati ya Real Madrid na Barcelona (El Classico) litapigwa mara tatu kabla hata ya msimu ujao wa ligi kuanza.

Kushinda kwa Barcelona kombe la Copa Del Rey kunamaanisha timu hizo mbili zitachuana katika mchezo wa Spanish Super Cup ambayo kwa kawaida huchezwa mara mbili nyumbani na ugenini.

Lakini bado tena mwezi wa July tarehe 28 mjini Miami Florida wababe hao watakutana katika fainali ya International Champions Cup hiyo nayo ikiwa ni bado ligi haijaanza.

Habari hii inaweza kuwa faraja kwa wapenzi wengi wa soka kwani ligi kwenda mapumzikoni zimefanya furaha ya wapenda soka kupungua kwa kiasi kikubwa.

 

Video: Walichofanya Azam FC kwa Bocco sio poa’– Shaffih Dauda

$
0
0

Timu ya soka ya Azam FC imeachana na mshambuliaji wake tegemeo wa muda mrefu John Raphael Bocco baada ya mkataba wake kumalizika, lakini ukweli ni kuwa tumezoea kuona wachezaji waliodumu kwa muda mrefu wakiagwa kwa heshima kitu ambacho hakijafanywa na Azam FC.

Mchambuzi wa michezo Shaffih Dauda ameguswa kwa namna ambavyo John Bocco ameondoka Azam FC na ametoa ushauri baada ya uongozi wa klabu hiyo kuthibitisha hawatakuwa na Bocco kuanzia msimu ujao na kuanzia sasa JB nimchezaji uru.

Unaweza kuangalia video hapa chini kwa story zaidi kuhusu kilakitu ambacho amekiongea Shaffih Dauda kuhusu issue ya John Bocco na Azam FC.


Tuzo za mchezaji bora wa Chelsea kwa msimu wa 2016/2017.

$
0
0

Baada ya msimu wa ligi 2016/2017kumalizika na Chelsea kuchukua ubingwa, usiku wa Jumapili waligawa tuzo kwa wachezaji bora waliofanya vizuri msimu huu.

Tuzo ambayo ilikuwa ikiangaliwa na wengi sana ilikuwa ni ya mchezaji bora wa timu hiyo msimu huu kutokana na Hazard na Kante kuwepo katika tuzo hiyo lakini Hazard alishinda tuzo hiyo.

Hazard hakuondoka na tuzo hiyo tu kwani bao alilowafunga Arsenal bado linakumbukwa katika klabu hiyo ambapo Chelsea wamempa Hazard kwa goli hilo kama goli bora la msimu.

Lakini Ngolo Kante hakuondoka hivi hivi kwani tuzo ya mchezaji bora kutokana na kura za wachezaji ilimuangukia na kumshinda Eden Hazard.

Lakini tukio hilo halikuisha kwa furaha sana kwani ilipokuja muda wa Terry kuaga ilionekana majonzi kutawala katika nyuso za wachezaji na wahudhuriaji wa tukio hilo.

Terry usiku huo alipewa tuzo ya utambulishi maalum na wakati wa kuaga alitoa hotuba fupi ambayo ilimgusa kila mchezaji na mashabiki wa Chelsea.

“Naamini nitarejea hapa siku moja, kwani nilishaambiwa milango iko wazi na hata kama naondoka hapa kwa sasa ila moyo wangu utakuwa umebaki hapa” alisema Terry katika sehemu ya hotuba yake hiyo.

 

Ona umwamba wa Fransesco Totti katika miaka.

$
0
0
  1. Huu ndio mwaka ambao kwa mara ya kwanza Totti alivaa jezi ya As Roma na kuanza kucheza soka, alikuwa kijana mdogo wa umri wa miaka 16 tu na mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Italia ulikuwa dhidi ya Brescia ambapo Roma walishinda kwa mabao 2 kwa 0.

1998.Alikuwa na umri wa miaka 21 tu na akaweka rekodi ya kijana mdogo wa kwanza kupewa cheo cha unahodha wa timu ya As Roma kwa mara ya kwanza kabisa.

2001.Huu ndio mwaka ambao Totti alibeba ubingwa wa ligi kuu Italia Serie A na huu ulikuwa ubingwa wake wa kwanza na wa mwisho wa ligi hiyo nchini Italia,akifunga goli katika ushindi wa mwisho wa 3 kwa 1 dhidi ya Parma.

2004.Alivunja rekodi ya Roberto Pruzzo ya ufungaji wa muda wote katika klabu ya As Roma baada ya kufikisha jumla ya mabao 169 na kuwa mfungaji bora wa muda wote katika klabu hiyo.

2006.Alicheza michezo yote 7 ya timu ya taifa katika kombe la dunia huku akifunga bao moja na kutoa assists zaidi ya tatu katika michuano hiyo mikubwa duniani.

2007.Alishinda tuzo ya kiatu cha dhahabu katika ligi kuu nchini Italia akiwa amefunga mabao 26 katika ligi hiyo huku mabao 32 akiwa amefunga katika michuano yote aliyocheza msimu huo.

2014.Aliweka rekodi ya mchezaji mkongwe zaidi katika champions league kufunga goli, kwania alifunga bao la kusawazisha dhidi ya Manchester City ikiwa ni siku moja tu baada ya kutimiza miaka 38.

2016.Alitokea katika benchi zikiwa zimebaki dakika 5 tu katika mchezo dhidi ya Torino, wakati anaingia Roma walikuwa wameshapigwa bao 2 kwa 1 lakini akafunga bao mbili na Roma wakamaliza na ushindi wa bak 3 kwa 2.

 

Totti Totti Totti jina linaloandikwa kila mahala mtandaoni.

$
0
0

Baada ya siku ya Jumapili mchezaji Fransesco Totti kucheza mchezo wake wa mwisho katika soka, watu mbalimbali wamekuwa wakimtumia salamu mchezaji huyo na kumuambia jinsi gani watamkumbuka.

Katika mtandao wa twitter kulikuwa na hashtag ya #Totti karibia kila ukurasa wa masuala ya soka duniani na hii ilionesha ni kwa jinsi gani Totti alikuwa akikubalika.

Mmoja kati ya watu ambao hawakusita kuonesha hisia zao mtandaoni ni mwanasoka Gervinho ambaye kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika “kati ya vitu ninajivunja ni kucheza na Totti,asante capitano mfalme wa Roma”

Lakini beki wa klabu ya Real Madrid Sergio Ramos amesema Totti kwa uwezo wake kila klabu duniani ingependa kuwa naye na akapost picha yake na kuandika Capitano.

Televisheni maarufu nchini Italia ya Itv imesema kupitia mtandao wa Twitter kwamba kuanzia sasa ligi kuu nchini Italia haitakuwa sawa kwani haiwezi kuwa sawa bila kuwepo kwa Fransesco Totti.

Klabu ya Inter Millan nayo imesema haiwezi kusahau jinsi Totti alibyokuwa akienda San Siro na watamkumbuka sana katika kipindi ambacho hayupo.

 

Video: Ushauri wa Shaffih Dauda kwa TFF baada ya ajali ya Mkude

$
0
0

Jana Mei 28, 2017 ilitokea ajali mbaya iliyomhusisha Jonas Mkude ambaye kiungo wa Simba na timu ya taifa ‘Taifa Stars’ pamoja na watu wengine ambapo shabiki mmoja wa Simba (Shose Fideline) alipoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa.

Baada ya ajali hiyo Shaffih Dauda ametoa ushauri kwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kutengeneza utaratibu maalum wa kuwafikisha wachezaji wa timu ya taifa kwenye kambi kutoka kwenye timu zao.

Kueleka UCL Final: Mambo 6 ya kuitia wasiwasi Madrid – dhidi ya Juve

$
0
0

Real Madrid wanauwinda ubingwa wa 12 wa kihistoria wa Champions League lakini kuna mambo 6 ambayo wanapaswa kuyaangalia kwasababu huenda yakawa kikwazo kwao. 
Mkosi wa bingwa mtetezi 

Endapo watafanikiwa kutwaa ubingwa wataweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wa CHAMPIONS LEAGUE – na kuushinda mkosi ambao umewahi kuzishibda timu 4 zilizokaribia kuvunja rekodi hiyo. 
Mnamo msimu wa 1993/94, AC Milan waliifunga Barcelona 4-0 katika fainali  kabla ya kuja kufungwa 1-0 na Ajax katika fainali ya msimu uliofuatia. Juventus nao wakaifunga Ajax katika fainali ua 1995/96 kwa mikwaju ya penati – Juventus nao wakashindwa kuutetea ubingwa kwa kufungwa na Borussia Dortmund miezi 12 baadae. 
Msimu wa 2007-08, Manchester United waliifunga Chelsea kwa penati na wao wakaja kupoteza miezi 12 baadae mbele ya Barcelona 

Mabingwa wa Klabu Bingwa ya Dunia

Tangu kuanzishwa kwa mashindanonya klabu bingwa ya dunia, haijawahi kutokea kwa mshindi wa michuano hiyo kwenda kubeba Champions League Trophy katika msimu huo huo. 

Mkosi wa mchezaji wa zamani 

Wachezaji wa zamani wa Real Madrid, Gonzalo Higuain na Sami Khedira, watakuwa katika kikosi cha Juventus na watapambana kwa kila hali kuweza kuidhuru timu yao ya zamani.  

Hata hivyo Juve nao watakuwa na pambano lao dhidi ya mkosi huu kwa Alvaro Morata ambaye aliwadhuru Madrid misimu miwili iliyopita timu hizi zilipokutana katika semifinal ya michuano hii. 
Mwaka Tasa 

Real Madrid hawajawahi kushinda ubingwa wa ulaya katika mwaka ambao haugawanyiki – mwaka tasa katika karne hii ya 21. Mara mwisho  kushinda Champions League ilikuwa mwaka 1959. 

Wapinzani wa Kiitaliano 

Historia inatuambia ni wakati wa kikosi cha kiitaliano kushinda UCL, kwa sababu kila baada ya miaka 7 kikosi cha waitaliano kimekuwa kikishinda Champions League – mara mwisho kwa waitaliano kushinda UcL ilikuwa miaka 7 iliyopita- Milan walibeba 2003 na miaka 7 nyuma mwaka 1996 Juventus walibeba. 

Jezi za Zambarau 
Madrid watakuwa ugenini katika mchezo huu wa fainali, hivyo watavaa jezi za Zambarau na katika msimu huu wamepoteza mechi mbili ambazo walivaa jezi hizo. 

Viewing all 9000 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>